Fuatilia hapa moja kwa moja Updates za mchezo huu kuanzia dakika ya kwanza hadi mwisho ili kujua kila kinachoendelea.
Mpira Umeanza - Simba SC 0-0 Turan PFK
Dakika ya 4 - Turan wanapata bao la Kwanza kupitia kwa Rodarik Miller kwa Mpira wa kona
Dakika ya 10 - Mpira ni wa kasi timu zote zikishambuliana
Dakika ya 20 - Simba wanapata faulo nje ya box baada ya Onana Kufanyiwa madhambi, Chama anaenda kupiga faulo inatoka nje
Dakika ya 40 - Mpira unaendelea huku timu zikishambuliana
Mapumziko - Simba SC 0-1 Turan PFK
Kipindi Cha pili Kimeanza
Dakika ya 47 - Mvua kubwa inashuka huku mchezo unaendelea
Dakika ya 48 - Sadio Kanoute anatoka Anaingia Fabrice Ngoma
Dakika ya 60 - Onana anakosa kutumia nafasi na mpira unadakwa na Kipa wa Turan Kamal
Dakika ya 63 - John Bocco anaingia akichukua nafasi ya Clatous Chama
Dakika ya 70 - Msako unaendelea tukiliandama lango la Turan PFK (mvua imeacha)
Dakika ya 80 - John Bocco anaunganisha krosi ya Mohammed Hussein Kipa wa Turan PFK Kamal anaokoa
Dakika ya 82 - Onana anatoka na kumpisha Jean Baleke
Dakika ya 85 - Jean Baleke anakosa goli la wazi baada ya kupokea pasi ya Mzamiru Yassin
Mpira umemalizika - Tumepoteza kwa bao 1-0