Fuatilia Mubashara kupitia App hiii kujua kinachoendelea
Kikosi tayari kimefika uwanjani.
Wachezaji wanapasha misuli moto.
Mchezo umeanza - Simba 0-0 Wadi Degla
Dakika ya 5 - Mechi inaendelea hakuna shambulizi la hatari kwa timu zote mbili
Dakika ya 10 - Wadi Degla Wanatengeneza shambulizi kwa kupigwa shuti ndani ya boksi na kipa, Camara anaupangua
Dakika ya 21 - Kona nzuri ya Ahoua inaunganishwa na kichwa na Mukwala iliyeunganisha vizuri ila kipa wa Wadi Degla anaudaka
Dakika ya 30 - Mapumziko mafupi (Water break)
Dakika ya 34 - Mechi inaendelea baada ya mapumziko mafupi
Dakika ya 37 - Mukwala anafunga bao ila mwamuzi anaamuru kuwa ni mpira wa kuotea.
Dakika 45 - Simba 0-0 Wadi Degla
Kipindi cha pili kimeanza kwa mabadiliko
Wametoka - Abraham na Mukwala
Wameingia - Bashiru na Sowah
Dakika ya 47 - Chasambi anatengeneza shambulizi, kwa kupiga pasi nzuri ya chini chini iliyomkuta Ahoua ndani ya boksi na kupiga shuti lililopaa juu ya lango.
Dakika 57 - Kona nzuri ya Mpanzu inaunganishwa na Chamou aliyepiga kichwa kizuri ila kipa wa Wadi anapangua na kuwa kona.
Dakika 58 - Kona nzuri ya Maema inaunganishwa kwa kichwa na De Rock ila mpira huo unatoka karibu na lango.
Dakika 73 - Eeeeeeeliiiieee Mpanzu mbele ya duara la katikati mwa kiwanja upande wa wapinzani anatandika shuti kali lililomshinda kipa wa Wadi aliyebaki anashangaa mpira huo uliotinga moja kwa moja nyavuni.
Dakika 74 - Mabadiliko Wanatoka Naby, Mpanzu na Maema Wanaingia, Abraham anaingia tena, Anthony Mligo na Joshua Mutale ‘Budo’
Dakika 78 - Ahoua baada ya kuwapiga chenga mabeki wawili wa Wadi waliogalagala chini anapiga pasi ya mwisho kwa Sowah aliyepiga shuti na kupaa juu ya lango.
Dakika 79 - Ahoua anapiga krosi nzuri anayomkuta Kibu akiwa ndani ya boksi akaunganisha kwa mtindo wa tikitaka kwa kutumia mguu wa kushoto na mpira huo kutinga moja kwa moja nyavuni.
Dakika 85 - Mechi inaendelea Simba 2-0 Wadi Degla
Mpira umemaliza - Simba Sc 2-0 Wadi Degla