Vikosi vyote vimeshafika uwanjani na vinapasha misuli moto kabla ya mchezo Kuanza'
Tayari timu zote zimeshakaguliwa muda wowote mchezo unaanza.
Dakika ya kwanza - Simba 0-0 Al-Adalah
3' - Ahoua anafanyiwa madhambi ndani ya boksi mwamuzi anakataa kutoa tuta
9' - Steven Mukwala anatuinua kwenye viti baada ya kupokea pasi ndefu kutoka kwa Fabrcie Ngoma
15' - Mchezo una kasi sana timu zote zikishambuliana kwa kasi
20' - Mpira mwingi unapigwa kati kati ya uwanja huku Fabrice Ngoma akiutawala mchezo
26' - mpira unachezwa burudani inamwagika sio ya kukosa ukiskia Ubaya Ubwela ndio huu
32' - Bao la pili bao hilo linatokana na pasi mpenyezo ya Ngoma, inayomkuta Mutale ndani ya boksi pembeni kulia mwa goli la mpinzani, anapiga shuti la kwanza linakwenda kugonga mwamba na mpira kumkuta tena baada ya kugonga mwamba, anapiga shuti la pili chinichini kushoto mwa kipa wa Al-Adalah nakuwa bao
40' - Simba 2-0 Al -Adalah
Kipindi cha kwanza kinamalizika Tupo mbele kwa Bao 2-0
46' - Mpira umeanza kipindi cha pili Simba 2-0 Al - Adalah
47' - Al- Adalah wanapata penati baada ya kipa Ally Salim kufanya madhambi ndai ya 18
47' - Al - Adalah 1-2 Simba
50 - Al-Adalah 1-2 Simba Mechi imebadilika na kuwa yenye ushindani huku wachezaji wa Al Adalah wakionekana kucheza rafu za mara kwa mara.
55' - Mukwala anafanya shambulizi la k ushtukiza na kupiga krosi ya chinichini inaokolewa na beki na kuwa kona.
60' - Simba 2-1 Al-Adalah
67' - Mabadiliko Anatoka - Mukwala - Anaingia - Mashaka
70' - Al-Adalah wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili kwa pamoja
72' - Mabadiliko Wanatoka - Mzamiru na Balua - Wanaingia - Awesu na Okejepha
80' -Mashaka kijana mdogo anasumbua beki ya Al- Adalah
85' - Mchezo unaendelea huku mechi ikiwa ngumu
86' - Mabadiliko Anatoka - Kapombe na Anaingia - Kijili
90' - Bado dakika 2 mchezo kuisha Simba 2-1 Al - Adalah
Mchezo umemalizika burudani nzuri kabisa chini ya Kocha Fadlu tukutane sasa kwenye ubaya ubwela jumamosi, Kama hujakata tiketi yako muda ndio huu usije kulaumu baadae