Simba Sports Club
News

Fetty Densa ataja siri ya ubingwa Simba Queens

14 May 2022

Fetty Densa amesema haikuwa kazi rahisi kutwaa ubingwa kutokana na upinzani uliopo lakini kujituma kwao na kufuata maelekezo ya walimu ndio siri ya mafanikio.

Fetty Densa ameongeza pamoja na kupata mafunzo mazuri kutoka kwa benchi la ufundi lakini mwalimu amekuwa akiwasisitiza kujituma uwanjani ili kufanikisha kutetea ubingwa jambo ambalo limekamilika jana.

"Ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi mara tatu mfululizo, haikuwa kazi rahisi lakini kujituma na kufuata maelekezo ya walimu ndio siri ya mafanikio," amesema Fetty Densa.

Advertisement

Fetty amewaomba mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani katika michezo miwili iliyobakia ukiwemo wa mwisho dhidi ya Baobab Queens ambao tutakabidhiwa ubingwa.

Queens ilitawazwa mabingwa jana baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mlandizi Queens ambao ulitufanya kufikisha pointi 57 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.

Back to homepage
Share this story