Fatuma anachukua nafasi ya Adam Moshi (Meja) ambaye amebadilishiwa majukumu na kupelekwa timu ya vijana.
Fatuma ana leseni C ya ukocha wa magolikipa inayojulikana na Mamlaka zote za soka ndani na nje ya nchi.
Kabla ya kujiunga na Simba Queens, Fatuma alikuwa kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Wanawake 'Serengeti Girls' pamoja na timu za taifa chini ya umri wa miaka 17 na 20 kwa muda wa miaka miwili.
Advertisement
Fatuma pia amewahi kuwa kocha wa makipa wa timu ya KMC inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC.
Fatuma anaungana na benchi la ufundi chini ya kocha mkuu, Charles Lukula kuiongoza Simba Queens kuhakikisha tunatetea taji letu la Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women's Premier League).