Simba Sports Club
News

Fadlu: Tupo tayari kwa Kombe la Shirikisho Afrika

11 Sep 2024

Kocha Fadlu ameyasema hayo akiwa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kuelekea Libya kwa ajili ya mchezo huo.

Kocha Fadlu ameongeza kuwa tunafahamu utakuwa mchezo mgumu lakini amewaandaa wachezaji kimwili na kiakili kuhakikisha tunafanya vizuri.

"Kama unavyoona tupo tayari kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, tunaelekea Libya tukiwa tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu," amesema Kocha Fadlu.

Advertisement

Akizungumzia kuhusu wachezaji waliokuwa kwenye timu za Taifa Kocha Fadlu amesema "ukiangalia wachezaji wote wamekuwa walipata nafasi Ally Salim, Mohamed Hussein na Edwin Balua wamekuwa wakianza kwenye kikosi cha Taifa Stars kama ilivyo kwa Steven Mukwala kule Uganda."

"Nyota wetu wote tutakutana nao kule Libya hii ina maanisha tutakuwa na kikosi chetu kamili," amemaliza kocha Fadlu.

Back to homepage
Share this story