Simba Sports Club
News

Fadlu Davids ndiye kocha wetu Mkuu

5 Jul 2024

Kabla ya kujiunga nasi msimu uliopita Fadlu alikuwa kocha Msaidizi wa mabingwa wa soka nchini Morocco Raja Club Athletic maarufu Raja Casablanca

Fadlu ambaye enzi zake alikuwa akicheza katika nafasi ya ushambuliaji anachukua nafasi ya Abdelhak Benchikha ambaye aliondoka wakati msimu wa 2023/24 ukiwa unaelekea ukingoni.

Mara nyingi Fadlu amekuwa muumini wa mfumo wa 4-2-3-1 ambao amekuwa akiutumia katika kila timu anayofundisha.

Fadlu analijua vema soka la Afrika kutokana na kuwahi kuzifundisha timu za Maritzburg United ya Afrika Kusini kwa nyakati tofauti pamoja na Orlando Pirates.

Advertisement

Mbali na kufundisha Afrika pia Fadlu amewahi kuwa Kocha Msaidizi wa Lokomotive Moscow ya Urusi.

Uongozi wa klabu unaamini uwezo alionao Fadlu utaweza kutufikisha katika malengo tuliyojiwekea katika msimu wa 2024/25.

Fadlu anataraji kuwasili Jumamosi hii akiwa na benchi lake lote la Ufundi tayari kuelekea Misri kwenye kambi ya Mazoezi (Pre Season)

Back to homepage
Share this story