Fadlu amesema tunaelekeza nguvu zote kwenye mechi nne za ligi zilizo mbele yetu na kuhakikisha tunapambana na kukusanya alama zote 12.
Akizungumzia mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane kutoka Morocco, Fadlu amesema utakuwa mchezo mgumu lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa ili kuwapa furaha Wanasimba.
Fadlu ameweka wazi kuwa tuna faida ya kumalizia mechi ya pili nyumbani katika Uwanja wa Benjamin Mkapa ambao tunaamini utakuwa na mashabiki 60,000 na hiyo ni moja ya silaha ambayo tunaitarajia.
"Baada ya kumaliza mechi ya nusu fainali ya pili jana sasa tunajiandaa na mechi za ligi kuu tuna michezo dhidi ya Mashujaa, JKT Tanzania Pamba Jiji na KMC FC ambazo tunahitaji kushinda zote."
"Kuhusu fainali nadhani tunahitaji kucheza vizuri ugenini ili tukija nyumbani Benjamin Mkapa iwe rahisi kwetu na matumaini yangu mashabiki watakuja kwa wingi kutupa nguvu," amesema Fadlu.