Fadlu amesema msimu uliopita tulikuwa na kikosi imara lakini kilifaa zaidi kwenye michuano ya ndani ingawa Kimataifa hatukuwa imara sana ila usajili tuliofanya mpaka sasa umezingatia mambo yote.
Fadlu amesema kuelekea msimu ujao tumeongeza ubora kwenye kila eneo ndani ya kikosi kuanzia idara ya ulinzi mpaka ushambuliaji.
"Ukimuangalia Rushine De Reuck ni mlinzi mwenye uzoefu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa, amecheza Mamelodi kwa mafanikio na tunategemea atakuwa msaada mkubwa kwetu. Moja eneo ambalo lilikuwa na mapungufu msimu uliopita ni hilo lakini ujio wa De Reuck utakuwa tiba."
"Katika eneo la kiungo ambalo ni roho ya timu tumewaongeza Allasane Kante na Hussein Daudi Semfuko ambao wataongeza nguvu hasa kwenye michuano ya Kimataifa."
Fadlu ameendelea na kusema "tumemsajili kiungo mshambuliaji Mohamed Bajaber ambaye anaweza kuongeza ufanisi katika eneo la juu. Bajaber ana uwezo mkubwa kufunga, kutoa usaidizi pamoja na kufungua timu pinzani ikiwa inajilinda."
Akizungumzia kuhusu idara ya ushambuliaji, Fadlu amesema nyota Jonathan Sowah atakuwa msaada mkubwa kwa timu kutokana na ubora pamoja na uzoefu alionao.
"Sowah ni mshambuliaji bora ambaye atakuwa msaada mkubwa kwa timu, anaweza kufunga na pia anajua jinsi ya kujipanga ili kuwatengenezea wengine nafasi na hilo litakuwa na faida kubwa kwa timu," amesema Kocha Fadlu.