Erasto amesema kila anaposhuka katika Uwanja wa Majimaji anakuwa na kumbukumbu nyingi sababu safari yake ya soka ndipo ilipoanzia.
Amesema anapokuja Songea marafiki zake, ndugu pamoja na jamaa hujitokeza kwa wingi uwanjani kumpa sapoti kitu ambacho kinampa furaha.
"Huku ni nyumbani najisikia furaha kucheza hapa, marafiki na ndugu zangu huja uwanjani kunitazama pia hapa ndipo historia yangu ya soka ilipoanzia.
Advertisement
"Nilikuja hapa mwaka jana katika mchezo wa nusu fainali ya FA dhidi ya Azam na leo nipo hapa tena na nitacheza mbele ya ndugu zangu," amesema Erasto.
Kiungo huyo amewaomba mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi uwanjani ili kutupa sapoti kuhakikisha tunashinda katika mchezo wa kesho wa kufungia msimu.