Simba Sports Club
News

Erasto awaita mashabiki kwa Mkapa Jumapili

11 Mar 2022

Erasto amesema uwepo wa mashabiki wengi uwanjani huwaongezea morali wachezaji na kujituma kuisadia timu kufanya vizuri.

Akizungumzia mchezo huo rasto ameongeza kuwa tumejipanga kuhakikisha tunashinda katika uwanja nyumbani ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kusonga mbele katika hatua inayofuata.

Advertisement

"Tunahitaji alama tatu muhimu nyumbani, maandalizi yetu ni mazuri na benchi la ufundi linaona mapungufu tunayofanya kila mechi na kuyafanyia kazi.

"Kikubwa nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kutupa sapoti tunaamini tutawapa furaha," amesema Erasto.

Back to homepage
Share this story