Balua ni mchezaji kijana mwenye miaka 23 amebarikiwa kuwa na kipaji kikubwa na tuna matumaini atakuwa msaada kwa timu.
Balua ambaye anatumia zaidi mguu wa kushoto anaweza kucheza kwa ufanisi winga zote, anaweza kucheza kama kiungo namba nane na kumi na wakati mwingine anacheza kama mlinzi.
Kipaji na umri aliokuwa nao ni moja ya sifa zilizotufanya kumsajili na kumtoa Mbeya hadi jijini Dar es Salaam.
Kutokana na uwezo wake huo alijumuishwa katika kikosi cha Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kilichocheza na Zanzibar Heroes katika mchezo wa kufungua Uwanja wa New Amaan Complex Zanzibar, Disemba 27 mwaka jana.
Balua anakuwa mchezaji wasita kusajiliwa katika dirisha dogo la usajili baada ya Saleh Karabaka, Babacar Sarr, Ladack Chasambi, Pa Omar Jobe na Freddy Michael Kouablan.