Simba Sports Club
News

Duchu akiri kukutana na mabadiliko kikosini

14 Jul 2023

Duchu amerejea kikosini akitokea Mtibwa Sugar alipokuwa kwa mkopo ambapo tayari amesaini mkataba mpya wa miaka miwili.

Duchu amesema amepokelewa vizuri na wachezaji wenzake tofauti na alivyotarajia huku akiweka wazi kuvutiwa na mazoezi tuliyoanza leo ikiwa ni siku ya kwanza ya maandalizi.

Duchu ameongeza kuwa anajiona mwenye deni kwa Wanasimba baada ya Uongozi kuonyesha imani kwakwe ya kumrejesha kikosini hivyo amejipanga kujituma kuhakikisha anapata nafasi ya kuisaidia timu muda mwingi.

Advertisement

"Kwanza mazoezi yamekuwa mazuri yameonyesha kweli tupo kwenye maandalizi, ninaamini wachezaji wengine wakifika kambi itazidi kuwa nzuri, hadi siku ya mwisho ikifika tutakuwa tayari kwa mashindano."

"Nimekutana na baadhi ya wachezaji niliyokuwa nao kwa mara ya mwisho na wengine wapya ila nimejihisi nipo nyumbani kuipambania timu na kuhakikisha natoa mchango wangu kila nikipata nafasi ili kufikia malengo yetu," amesema Duchu.

Back to homepage
Share this story