Simba Sports Club
News

Droo hatua ya makundi Afrika kupangwa Desemba 28

16 Dec 2021

Droo ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi imepangwa kufanyika Jumanne Desemba 28, mwaka huu.

Droo hiyo itafanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yaliyopo Cairo, Misri kuanzia saa saba mchana na itarushwa moja kwa kwenye mitandao ya kijamii ya Shirikisho hilo.

Timu 16 ambazo zimeingia hatua hiyo zitagawanywa katika makundi manne ambayo kila moja litakuwa na timu nne. Hatua ya makundi ya michuano hiyo inatarajia kuanza Februari mwakani.

Advertisement

Hizi hapa timu 16 zilizofuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika

Al Ahli Tripoli (Libya), Al Masry (Misri), AS Otoho (Congo), ASEC Mimosas (Ivory Coast), Coton Sport (Cameroon), CS Sfaxien (Tunisia), JS Saoura (Algeria), Orlando Pirates (South Africa), Pyramids (Misri), RS Berkane (Morocco), Simba (Tanzania), TP Mazembe (DR Congo), US Gendarmerie Nationale (Niger), Zanaco (Zambia), Al Ittihad (Libya) OR Enyimba (Nigeria), JS Kabylie (Algeria) OR Royal Leopards (Eswatini).

Back to homepage
Share this story