Simba Sports Club
News

Dkt Mwigulu Aunga Mkono Kampeni ya Kataa Feki Vaa Orijino

12 Oct 2025

Licha ya kununua jezi hizo lakini pia Dkt. Nchemba amewataka mashabiki kununua bidhaa za klabu kwani kwa kufanya hivyo wanasaidia kuinua uwezo wa kifedha wa klabu jambo ambalo linaisaidia taasisi kujiendesha kikamilifu.

Pia Dkt. Nchemba amepongeza ziara ambayo tunaendelea kuifanya ya kutoa elimu kwa mashabiki wetu na kuzishauri taasisi zingine kujifunza kwa Simba namna ambavyo tunawafuata mashabiki wetu katika maeneo yao ili kuwapa elimu.

Advertisement
Back to homepage
Share this story