Simba Sports Club
News

Djafar, Bukuru wajiunga Simba Queens

11 Dec 2023

Nyota hao wamejiunga na timu na wameshiriki mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii tutakayocheza kesho na JKT Queens katika Uwanja wa Azam Complex.

Queens ambayo inanolewa na Kocha Juma Mgunda akisaidiwa na Mussa Hassan Mgosi imefanya mazoezi hayo katika Uwanja wa Mbweni Veterani ambapo wachezaji wote wameshiriki na wapo kwenye hali nzuri.

Advertisement

Tunawaheshimu JKT na tunajua ni mabingwa watetezi lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuchukua taji la Ngao ya Jamii.

Back to homepage
Share this story