Simba University Bonanza imeshirikisha timu 14 kutoka katika Vyuo mbalimbali vilivyopo jijini Dar es Salaam lengo likiwa kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya CS Sfaxien kutoka Tunisia.
Katika mchezo huo wa fainali bao pekee limefungwa na nahodha wa Diplomasia Dicey Dickence kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji mmoja wa St. Joseph kuunawa mpira ndani ya 18.
Hii ni mara ya kwanza kwa Bonanza kuelekea mechi zetu za Kimataifa kushirikisha timu kutoka kwenye vyuo mbalimbali kutoka Dar es Salaam.
Vyuo zilivyoshiriki kwenye Bonanza la mwaka huu ni Uhasibu, Bandari, DIT, IFM, DSJ, Utumishi wa Umma, Chuo cha Diplomasia, St. Joseph Mbezi, Kampala University, Ustawi wa Jamii, St. Joseph Afya, CBE, Tumaini University na City College.
Katika Bonanza hilo mchezaji bora ni nahodha wa Diplomasia Dicey Dickence ambaye pia ni mfungaji bora baada ya kutupia kambani mabao matatu.
Michael Kazikulima kutoka chuo cha Diplomasia ameibuka mlinda mlango baada ya kutoka na Clean Sheet kwenye mechi nne.