Kabla ya kujiunga nasi kocha Pantev alikuwa akikinoa kikosi cha Gaborone United ya Botswana ambayo tulikutana nao kwenye mchezo wa hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika wiki iliyopita.
Pantev (49) ana uzoefu na soka la Afrika ambapo amefundisha na kushinda mataji katika ligi mbali mbali ikiwemo Cameroon akiwa na Victoria United (2023/2024) na Botswana akiwa na Gaborone United(2024/2025).
Advertisement
Pantev ni muumini wa kucheza soka la kushambulia na kuzuia huku akipenda kumiliki mchezo kama ilivyo falsafa ya Simba.
Pantev atawasili jijini Dar es Salaam kesho tayari kuanza kukinoa kikosi ambacho kitarejea mazoezini siku ya Jumatatu.