Simba Sports Club
News

Dilunga awapa neno mashabiki kuelekea mechi zijazo

30 Jan 2022

Kiungo mshambuliaji Hassan Dilunga, amewaomba mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuisapoti timu huku wao kama wachezaji wakiahidi kuwapa furaha.

Dilunga amesema baada ya kipindi kigumu kupita cha kushindwa kupata matokeo upepo umeanza kurejea na siku za furaha zitarudi tena kama kawaida.

Nyota huyo ameongeza kuwa amefurahi kuwepo katika kikosi kilichopata ushindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Dar City na anaamini tutaendelea kushinda kuanzia sasa.

Advertisement

Akizungumzia mchezo unaofuata wa hatua ya 16 bora wa Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Ruvu Shooting, Dilunga amesema tutajipanga kuhakikisha tunashinda na lengo kuu ni kutetea ubingwa.

"Nimefurahi kuwa sehemu ya kikosi kilichopata ushindi baada ya kupitia kipindi kigumu, mashabiki wetu waendelee kujitokeza kwa wingi uwanjani kutupa sapoti sisi tutawapa furaha.

"Sisi ni mabingwa watetezi wa michuano hii, tunaenda kukutana na Ruvu Shooting tutajipanga kuhakikisha tunashinda ili tuvuke hatua inayofuata na hatimaye tutetee taji letu," amesema Dilunga.

Back to homepage
Share this story