Simba Sports Club
News

Dilunga arejea Kikosini

14 Mar 2023

Dillunga alipata majereha ya goti Februari mwaka jana na kufanyiwa upasuaji Juni nchini Afrika Kusini na kwa mujibu wa maelekezo ya kitabibu alitakiwa kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi nane ili kuuguza jeraha lake .

Baada ya kukaa nje kwa kipindi hicho hatimae leo hii kiungo huyo fundi amejiunga na kikosi na kuanza mazoezi chini ya uangalizi wa madaktari.

Daktari wa timu Edwin Kagabo amesema mazoezi ya leo ilikuwa ni kumfanyia uchunguzi ili kuangalia kwa namna gani ameanza kuimarika.

"Dilunga amerejea kikosini na anafanya mazoezi chini ya uangalizi na hali yake ni imeimarika kwa kiasi kikubwa lakini bado tunaendelea kumchunguza," amesema Dk. Edwin.

Advertisement

Dilunga hakuwa miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa msimu huu hivyo ataendelea kufanya mazoezi hadi mwisho wa msimu huku jopo la madaktari likiendelea kumfanyia tathmini na matibabu.

Endapo afya yake itaendelea kuimarika kama ilivyo sasa basi Dilunga atasajiliwa kwa ajili ya matumizi ya msimu ujao.

Uongozi wa klabu umefurahishwa na kurejea wa Dilunga kwani ni mchezaji muhimu ndani ya kikosi.

Back to homepage
Share this story