Debora anamudu pia kucheza kama kiungo mkabaji namba sita ingawa anafurahi zaidi kucheza juu kidogo yaani namba nane.
Ujio wa Debora unaongeza nguvu katika eneo letu la kiungo kwakuwa anaweza kuzuia na kupiga pasi sahihi kuelekea mbele na kuanzisha mashambulizi.
Advertisement
Tunaendelea kusuka timu imara kwa ajili muda mrefu ndio maana usajili wetu umezingatia umri wa wachezaji tunaowasajili.
Debora anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa katika idara ya kiungo wa kati baada ya jana kumsajili Augustine Okajepha lengo likiwa ni kuongeza uimara wa kikosi.