Danai alikuwepo kwenye kikosi cha Queens kilichoibuka na ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women's Premier League (SLWPL) msimu wa 2020/21.
Pia Danai alikuwepo katika kikosi cha Queens kilichoshiriki michuano ya CECAFA SAMIA CUP iliyofanyika nchini Kenya mwaka 2021.
Advertisement
Danai anaungana na wazoefu Mwanahamisi Omary 'Gaucho' na Asha Rashid 'Mwalala' tuliowasajili katika dirisha dogo kuongeza nguvu kikosini.
Usajili wa nyota hao unaendana na malengo ya timu ya kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya CECAFA itakayotupa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.