Mchezo ulianza kwa kasi huku dakika ya kwanza mshambuliaji Seleman Mwalimu alipoteza nafasi ya wazi baada ya kupokea pasi kutoka kwa Libasse Gueye lakini mlinda mlango Aishi Manula alikuwa imara.
Azam nao walijaribu kufika langoni kwetu mara kadhaa kipindi cha kwanza lakini safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara huku mlinda mlango Djibrilla Kassali akiwa kikwazo kwao.
Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi huku tukitengeza nafasi nyingi za kufunga lakini hata hivyo ufanisi wetu kwenye kuzitumia haikuwa mzuri.
Matokeo haya yanatufanya kuendelea kusalia nafasi ya pili kwenye msimamo kwa kufikisha alama 35 baada ya kucheza mechi 16.
X1: Manula, Mwaikenda, Msindo, Twalib, Fuentes, Himid, Abah (Diakite 55'), Akaminko, Saadun (Kanoute 66'), Fei Toto (Ngita 80'), Nado (Mzee 55')
Waliionyeshwa kadi: Msindo 26' Twalib 34'
X1: Kassali, Kapombe, Kibabage, Toure, De Reuck, Kagoma, Gueye, Kante, Mwalimu, Chama (Maema 63'), Oura
Waliionyeshwa kadi: Kapombe 30' Chama 39'