Simba Sports Club
News

Crescentius Magori Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi

4 Sep 2025

Awali Mo alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi lakini kutokana na shughuli zake kuwa nyingi ameamua kuiachia nafasi hiyo kwa Magori ambaye atakuwa na muda mwingi kuwatumikia Wanasimba.

Katika barua yake aliyotoa kwa Vyombo vya Habari Mo amesema Bodi ya Wakurugenzi inahitaji mtu ambaye ataweza kuiongoza kwa ukaribu huku yeye akiendelea kubaki kama Rais wa heshima na ameona Magori kuwa mtu sahihi.

Mbali na kumteua ndugu Magori pia Mo ametangaza Wajumbe wapya wa Bodi wa Wakurugenzi huku akimrejesha aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Klabu (CEO) Barbara Gonzalez kama Mjumbe na aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu, Swedi Mkwabi.

Hawa hapa Wajumbe wapya wa Bodi ya Wakurugenzi waliotanagazwa:

1. Barbara Gonzalez

2. Hussein Kitta

Advertisement

3. Azim Dewji

4. Swedi Mkwabi

5. Rashid Shangazi

6. Zuly Chandoo

7. George Ruhago

Back to homepage
Share this story