Simba Sports Club
News

CRDB, Yas wadhamini wa mchezo wetu wa Nusu Fainali

15 Apr 2025

Meneja Habari na Mawasiliano wa Klabu, Ahmed Ally amesema CRDB na Yas hawatajutia kudhamini mchezo huo kwakuwa Simba ni kubwa na itawafikia watu wengi.

Aidha Ahmed ameyakaribisha makampuni pamoja na Taasisi nyingine kuendelea kujitokeza kudhamini mchezo huo kwakuwa itakuwa ni fursa kubwa kwao.

“Mechi hii ya nusu fainali ina wadhamini wake maalumu, nipende kuwatangaza CRDB Bank na tumekuwa nao tangu mwanzoni kwenye michuano hii na tuwambie tu hatutawaangusha tutakwenda hadi fainali. Lakini pia tupo na mtandao wa Yas, wametudhamini ili tuwe na mazingira mazuri ya kwenda fainali. Kampuni yeyote ambayo inataka kuidhamini Simba kwa mechi ya nusu fainali, milango ipo wazi," amesema Ahmed.

Advertisement

Ahmed pia ametoa utaratibu pia wa zoezi la hamasa litakalofanyika Jumamosi, Aprili 19 Visiwani Zanzibar.

“Jumamosi tutaamkia Mtoni Kidatu, tutatembelea vijiwe vya kahawa vile vya Simba tu kwenda kuwakaribisha kwenye mchezo wetu. Tutafunga siku kwenye tawi la Kikwajuni, hili ni tawi la kwanza la Simba la Tanzania nzima,” amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story