Simba Sports Club
News

Chlouha Zakaria Kocha mpya wa Makipa

15 Nov 2022

Zakaria (52) amejiunga nasi akitokea klabu ya Dibba Al Fujaira kutoka Falme za Kiarabu (UAE).

Zakaria unachukua nafasi ya Mohamed Rachid ambaye mkataba wake ulisitishwa na Uongozi wa klabu Septemba 9, mwaka huu.

Zakaria pia amewahi kuinoa timu ya Al Batech Club kutoka huko huko Falme za Kiarabu kwa miaka miwili tangu 2019 hadi 2021.

Ujio wa Zakaria ni moja ya mipango ya kuliboresha benchi la ufundi kuelekea kuanza kwa hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Advertisement

Akiwa mchezaji Zakaria amezichezea timu zote kubwa za Morocco Raja na Waydad Casablanca.

Msimu wa 2008/9 Zakaria alifika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa na miamba, Wydad Casablanca.

2009/10 alifanaikiwa kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu nchini Morocco akiwa na Wydad.

2010/11 akiwa Kocha wa magoli kipa wa Wydad alifanikiwa kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo walicheza dhidi ya Esparance De Tunis.

Back to homepage
Share this story