Che Malone amesema wachezaji hawaridhishwi na hali ya kikosi ilivyo kwa sasa wanahitaji kuipambana ili kurejesha timu katika hali ya ushindi.
Che Malone amewaomba mashabiki kuendelea kuipa sapoti timu na wasivunjike moyo kutokana na matokeo mabaya tuliyopata katika mechi mbili zilizopita badala yake tuwe kitu kimoja.
Advertisement
"Sisi wachezaji tupo tayari kuhakisha tunapata ushindi katika mchezo wa kesho dhidi ya ASEC. Tunafahamu mashabiki hawana furaha lakini ni wakati wa kuwa pamoja ili tuvuke kwenye hali hii.
"Tutahakikisha tunapata matokeo chanya ili kurejesha hali ya kujiamini lakini tunahitaji sapoti kutoka kwa mashabiki," amesema Che Malone.