Nyota hao ni mlinzi wa kati, Che Fondoh Malone kiungo, Willy Essomba Onana pamoja na mshambuliaji, Jean Baleke.
Nyota hao wanatarajia kufika Uturuki leo usiku na kesho moja kwa moja wataanza programu ya mazoezi.
Advertisement
Kiungo mshambuliaji Aubin Kramo Kouame yeye ataungana na kikosi moja kwa moja leo mchana akitokea nchini kwao Ivory Coast baada ya kuanza safari ya kuelekea Uturuki jana.
Kiungo mkabaji Fabrice Luamba Ngoma yupo jijini Dar es Salaam akimalizia taratibu za vibali vya kuingia Uturuki na anategemea kujiunga na wenzake baadae wiki hii.