Simba Sports Club
News

Che Malone aridhishwa na kambi ya Misri

14 Jul 2024

Che Malone amesema mpaka sasa kambi imefikisha wiki moja lakini wachezaji wanashika vizuri mafunzo ingawa idadi kubwa ni wageni kikosini.

Akizungumzia benchi jipya la ufundi Malone amesema "wanatusaidia kuanzia uwanjani hadi ushauri wa jinsi gani ya kuishi nje ya uwanja.

Advertisement

"Wachezaji wengi ni wageni lakini wanaonekana kuzoea haraka mazingira na wanashika vizuri mafunzo, tuna imani tutafanya vizuri msimu ujao. Kila mmoja wetu yupo tayari kufanikisha malengo ya klabu," amesema Che Malone.

Akizungumzia kuhusu msimu ujao Che Malone amesema "utakuwa mgumu zaidi ya uliopita kutokana na timu nyingi kujipanga vizuri kusajili wachezaji bora."

Back to homepage
Share this story