Simba Sports Club
News

Chama: Tuko tayari kwa Ruvu Shooting

16 Feb 2022 By simbasc 1,287 views

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amesema wachezaji wote wamejipanga tayari kwa mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo wa hatua ya 16 bora wa Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) utapigwa leo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Chama amesema wachezaji wana ari ya hali ya juu na kila mmoja anatambua umuhimu wa mchezo akitambua lengo ni kushinda na kufuzu robo fainali.

Advertisement

Chama ameongeza kuwa mchezo utakuwa mgumu na Ruvu Shooting mara zote wamekuwa wakitusumbua lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

"Kwa upande wetu wachezaji tuko kamili, tuko tayari kutimiza maagizo tutakayopewa na benchi la ufundi na kila atakayepata nafasi atakuwa atapeperusha vema bendera ya Simba," amesema Chama.

Back to homepage
Share this story