Simba Sports Club
News

Chama, Mugalu, Morrison waanza mazoezi Mkude apumzishwa

10 May 2022

Wachezaji hao watatu wameukosa mchezo wetu wa juzi dhidi ya Ruvu Shooting tuliobuka na ushindi wa mabao 4-1.

Wakati Chama, Mugalu na Morrison wakianza mazoezi kiungo mkabaji Jonas Mkude amefanyiwa vipimo kuangalia maumivu aliyopata katika mchezo na amepewa mapumziko ya siku mbili akisubiri majibu ya vipimo.

Advertisement

Mkude aliumia dakika ya 20 na kushindwa kuendelea na mchezo huo na majibu ya vipimo yakitoka ataanza matibabu mara moja ingawa inaonekana hajapata majeraha makubwa.

Back to homepage
Share this story