Simba Sports Club
News

Chama mchezaji bora wa mashabiki Desemba

4 Jan 2023 By simbasc 457 views
Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month). Chama amewashinda Nahodha John Bocco na mlinzi Shomari Kapombe ambao alikuwa ameingia nao fainali kwenye kinyang'anyiro hicho. Katika mwezi Desemba, Chama amecheza dakika 540 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine saba. Mchanganuo wa kura ulivyokuwa Kura            Asilimia Chama             1829            54.52 Bocco               1415            42.18 Kapombe           111              3.31 Kwa kuibuka mshindi Chama atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.
Advertisement
Back to homepage
Share this story