Simba Sports Club
News

Chama Mchezaji Bora wa Mashabiki Agosti

5 Sep 2022

Chama amewashinda viungo wenzake Pape Sakho na Sadio Kanoute ambao aliingia nao fainali kwenye kinyang'anyiro hicho.

Chama ameshinda kutokana na kupata kura nyingi kutoka kwa mashabiki zilizopigwa kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz kuanzia Agosti 29 hadi Septemba Mosi.

Kwa ushindi huo Chama atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa

Kura Asilimia Nafasi

Advertisement

Chama 1551 60.30 1

Sakho 506 19.63 3

Kanoute 516 20.06 2

Katika mwezi Agosti Chama amecheza mechi zote tatu sawa na dakika 231 akifunga bao moja na kusaidia kupatikana kwa mengine matatu.

Back to homepage
Share this story