Simba Sports Club
News

Chama, Inonga warejea kuiwahi Dodoma Jiji Jumapili

30 Sep 2022

Chama alikuwa na kikosi cha Timu ya Taifa ya Zambia 'Chipolopolo' wakati Henock alikuwa na DRC katika mechi za kirafiki za kimataifa zilizopo kwenye kalenda ya FIFA.

Wawili hao wanaungana na wenzao ambao wameingia kambini jana kutoka Visiwani Zanzibar tulipokuwa na kambi ya wiki moja ambapo tulicheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Malindi SC na Kipanga FC.

Nyota wengine waliokuwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kilichokwenda Libya, Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yassin na Habib Kyombo nao wamejiunga na wenzao kambini.

Viingilio vya mchezo wa Jumapili vitakuwa kama ifuatavyo:

Advertisement

Mzunguko Sh 5,000

VIP B na C Sh 10,000

VIP A Sh 15,000

Back to homepage
Share this story