Nyota hao ni viungo washambuliaji, Clatous Chama (Zambia 'Chipolopolo') na Said Ntibazonkiza (Burundi 'Intamba Murugamba') na mlinzi wa kati, Henock Inonga (DRC Congo).
Chama atakiongoza kikosi cha Zambia kinajiandaa na mchezo dhidi ya Comoros utakaopigwa Septemba tisa.
Advertisement
Ntibazonkiza atakuwemo kwenye kikosi cha Intamba Murugamba' kitakachoikabili Cameroon.
Wakati Inonga ambaye hali yake ya kiafya imezidi kuimarika kutokana na kuumia bega kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii atakuwa katika kikosi cha DR Congo ambacho kitacheza dhidi ya Sudan.