Nyota hao ni kiungo mshambuliaji, Clatous Chama na walinzi Che Fondoh Malone pamoja na Shomari Kapombe.
Katika mwezi Septemba tumecheza mechi mbili ambazo ni dhidi ya Power Dynamos ugenini pamoja mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union.
Hizi ndio takwimu zao wote:
Dakika Magoli Assist
Chama 180 2 1
Advertisement
Che Malone 180 0 0
Kapombe 162 0 0
Zoezi la kupiga kura kupitia kwenye tovuti ya klabu ya www.simbasc.co.tz limeanza tayari na litafungwa Jumatano Oktoba 11 saa sita usiku.
Mshindi wa jumla atakayepata kura nyingi atapokea pesa taslimu Sh. 2,000,000 kutoka kwa Uongozi wa klabu.