Simba Sports Club
News

Chama, Bocco, Kapombe kuchuana mchezaji bora Desemba

31 Dec 2022

Wachezaji hao ni kiungo mshambuliaji Clatous Chama, Nahodha John Bocco na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

Awali walikuwa watano pamoja na viungo Mzamiru Yassin na Pape Sakho lakini baada ya mchujo wamebaki nyota hao watatu.

Katika mwezi Desemba tumecheza mechi sita tumeshinda tano na kutoka sare moja huku nyota hao wakiwa ufunguo wa ushindi huo.

Mchanganuo wa takwimu zao za mwezi Desemba

Dakika Magoli Assist

Advertisement

Chama 540 4 7

Bocco 422 5 0

Kapombe 505 1 3

Zoezi la kupiga kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz litaanza leo saa 6:00 mchana na litakamilika Januari 2 saa 6:00 mchana.

Mshindi atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile kama sehemu ya zawadi.

Back to homepage
Share this story