Simba Sports Club
News

Chama azidi kung'ara Ligi ya Mabingwa Afrika

7 Apr 2021 By simbasc 2,074 views

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama amechaguliwa mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa Afrika mzunguko wa tano kutokana na kiwango bora alichokionyesha katika mchezo wetu dhidi ya AS Vita uliopigwa Aprili 3, mwaka huu.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Chama alifunga mabao wawili na kusaidia kupatikana kwa ushindi wa 4-1.

Advertisement

Chama raia wa Zambia amewashinda Amiri Sayoud (CR Belouizdad) Ricardo Goss (Mamelod Sundowns) na Ferjan Sassi (Zamalek) kwa kupata asilimia 51 ya kura zilizopigwa.

Chama anakuwa mchezaji wa pili kutoka kwenye kikosi chetu kuchaguliwa mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa baada ya Luis Miquissone kufanya hivyo mwezi uliopita.

Back to homepage
Share this story