Chama amesema kupoteza mechi mbili dhidi ya Horoya na Raja Casablanca kusiwafanye mashabiki kuvunjika moyo kwa kuwa wachezaji wanaamini wanaweza kupindua meza na kufanya vizuri.
"Ni kweli hatukuanza vizuri hatua ya makundi lakini mashabiki wetu wasikate tamaa. Sisi wachezaji tunaamini tunaweza kubadili upepo mambo yakawa vizuri.
Advertisement
"Walimu wetu wametuelekeza mambo mengi na wamejaribu kuondoa mapungufu yaliyojitokeza kwenye mechi zilizotangulia," amesema Chama.
Akizungumzia mchezo unaofuata dhidi ya Vipers, Chama amesema; "utakuwa mgumu, tunajua Vipers nao hawajapata matokeo mazuri kwenye mechi zao lakini tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunashinda."