Chama alisafiri na kikosi kilichopo jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Yanga Jumamosi katika Uwanja wa CCM Kirumba.
Ingawa tayari alikuwa ameanza mazoezi mepesi lakini juzi alipelekwa hospitali ya Bugando na vipimo vimeonyesha anahitaji kupata matibabu zaidi.
Chama ameondoka jana usiku kurejea Dar Es Salaam na moja kwa moja ataelekea Zambia kwenye maadhimisho ya mwaka mmoja wa kifo cha mkewe ambayo itafanyika May 28 Nchini Zambia
Advertisement
Baada ya kushiriki ibada hiyo Chama ataendelea na matibabu akiwa kwao Zambia kabla ya kurejea tena Tanzania kujiunga na timu
Chama anaungana na viungo wengine Jonas Mkude na Hassan Dilunga ambao ni majeruhi na wataukosa mchezo wa Jumamosi.