Simba Sports Club
News

Chama arejea, kucheza dhidi ya Ruvu Shooting leo

19 Nov 2022 By simbasc 260 views
Kiungo mshambuliaji Clatous Chama amerejea kikosini katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting baada ya kukosekana kwenye mechi tatu kutokana na kutumia adhabu. Kocha Juma Mgunda amempanga Chama kushambulia kutokea pembeni pamoja Augustine Okrah kwa sababu leo ameanza na washambuliaji wawili. Baada ya kukosekana kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi, Nahodha John Bocco ataongoza mashambulizi pamoja na kinara Moses Phiri. Kikosi Kamili Kilivyopangwa Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Augustine Okrah (27). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Nassor Kapama (35), Kibu Denis (38).
Advertisement
Back to homepage
Share this story