Wawili hao wataondoka kesho mchana kwa Ndege ya moja kwa moja kutoka jijini Dar es Salaam hadi Doha nchini Qatar tayari kwa upangaji wa droo hiyo.
Katika droo hiyo Simba tunategemea kupangwa na kati ya timu tatu ambazo ni
Al Masry (Misri) ASEC Mimosas (Ivory Coast) na Stellenbosch (Afrika Kusini).
Hii inatokana na sisi kumaliza vinara wa kundi letu huku timu tajwa hapo juu nikimaliza nafasi ya pili kwenye makundi yao.
Droo hiyo itahusisha timu nane zilizofuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ambazo ni Zamalek SC (Misri), Asec Mimosas (Ivory Coast), Al Masry (Misri ), CS Constantine (Algeria), RS Berkane (Morocco), Simba SC (Tanzania), Stellenbosch FC (Afrika Kusini), USM Alger (Algeria).
Droo hiyo ambayo itafanyika katika mji wa Doha itaanza saa 11 jioni kwa saa za Tanzania.