Simba Sports Club
News

CEO Kajula aweka wazi mipango ya Utendaji wake

29 Jan 2023

Kajula amesema jambo la kwanza atakalofanya ni kuhakikisha anaiunganisha klabu kuanzia Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti, Wanachama mpaka mashabiki.

Katika siku yake ya kwanza ofisini ambayo itakuwa kesho Jumatatu, Januari 30 Kajula amepanga kwenda kuwatembelea wadhamini wetu.

Kajula amesema miongoni mwa vitu atakavyo visimamia ni:

- Kuhakikisha wakati mwingine tutafanya Mkutano Mkuu wa kiteknolojia utakaowahusisha wanachama wote nchi nzima.

- Tutajenga timu imara kwa ajili ya mataji. Kuboresha benchi la Ufundi.

Advertisement

- Tutaimarisha brand ya klabu yetu na kuitumia vizuri kutuongezea kipato.

- Kusimamia ujenzi Hosteli za kisasa na tayari mchoro umekamilika.

- Kuboresha Sherehe za Simba Day

- Kuunganisha matawi kote nchi nzima

Back to homepage
Share this story