Lengo la ziara hiyo ni kujenga mahusiano mazuri na Taasisi pamoja klabu za mpira ili kukuza ushirikiano na kubadilishana uzoefu katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
Akiwa makao makuu ya miamba hiyo nchini Afrika Kusini, CEO Kajula amekutana na Mwenyekiti wa Sundowns, Tihopie Motsepe, Mkurugenzi wa Ufundi Flemming Berg na Mkuu wa Mashindano Stanley Mabulu.
Viongozi hao wamejadiliana mambo mbalimbali ya maendeleo ya soka, miundo mbinu yake na jinsi kujikwamua kutoka tulipo hadi kufika ngazi za juu ambazo tunataka kufika.
Kwakuwa lengo letu ni kuwa moja ya klabu kubwa barani Afrika katika siku za baadae tunazidi kufanya ushirikano na wenzetu walioendelea ili kujifunza mambo mengi ili siku moja tuwafikie.
Mwezi uliopita tuliwaalika Al Hilal ya kuwawezesha kupata kambi ya wiki mbili kujiandaa na michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa ni sehemu ya ushirikiano tulionao na miamba hiyo ya Sudan.
Wakiwa Tanzania Al Hilal walipata mechi tatu za kirafiki dhidi ya Namungo, Azam FC na sisi wenyewe ambao tuliwaandalia kila kitu.