Simba Sports Club
News

CEO Kajula akutana na Wachezaji

2 Feb 2023

Kajula amewasisitiza wachezaji kuendelea kujituma na kuwa nidhamu nzuri baina yao na benchi la ufundi ili umoja na mshikamano uwepo ambao utachangia furaha kwetu sote.

Kajula amewaambia wachezaji kuwa Wanasimba wanahitaji furaha ya kurejesha mataji yaliyopotea msimu uliopita lakini wao ndio wenye uwezo wa kutimiza azma hiyo.

"Nimefurahi kukutana nanyi na kuongea mambo machache, kikubwa nawasisitiza furaha ya Wanasimba ipo miguuni kwenu.

Advertisement

"Tunahitaji kurejesha mataji pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hilo litawezekana endapo nyinyi mtatimiza majukumu yenu uwanjani.

"Nasi kama Menejimenti tutahakikisha mnapata kila kitu ambacho mnastahili kukipata kwa wakati ili lazi yenu iwe kufikiria uwanjani," amesema Kajula.

Back to homepage
Share this story