Rufa raia wa Kenya alipata majeraha hayo katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Cecafa Dhidi ya Kenya Police Bullets iliyofanyika nchini Ethiopia, Agosti mwaka huu.
Daktari wa Simba Queens, Naima Mohamed amesema upasuaji huo utamfanya Rufa kukaa nje ya uwanja kwa miezi nane kabla ya kurejea dimbani hivyo msimu mzima utaukosa.
Advertisement
"Upasuaji umeenda vizuri na matarajio yetu ni kwamba baada ya kupona atakuwa tayari kurudi Uwanjani," amesema Dkt. Naima.