Camara alifanyiwa upasuaji wa goti, Novemba 16 mwaka huu ambapo alipewa siku 10 za uangalizi wa madaktari wa hospitali jijini Casablanca ili kujiridhisha kama yuko sawa na anastahili kuruhusiwa.
Baada ya kurejea Camara ataendelea kubaki chini ya uangalizi wa ili matibabu yakamilike kama inavyopaswa kwa mujibu wa maelekezo ya daktari.
Advertisement
Camara alipata majeraha hayo katika mchezo wa mkondo wa pili wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 28.