Camara atafanyiwa upasuaji siku ya Jumatatu Novemba, 17 na anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki nane mpaka 10.
Camara alipata majeraha hayo katika mchezo wa mkondo wa pili wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 28.
Advertisement
Katika mchezo huo uliomlizika kwa sare ya kufungana bao moja Camara alishindwa kuendelea na kufanyiwa mabadiliko dakika ya 77.