Cadena amesema tuliweza kumiliki mchezo na kufanya mashambulizi mengi na kutengeneza nafasi ingawa hatujapata tulichotarajia.
Cadena ameongeza kuwa jambo chanya ni kwamba wachezaji wameshika haraka mafunzo aliyowapa kitu ambacho anaamini katika mechi za mbeleni tutafanya vizuri.
Advertisement
"Sijafurahia matokeo ya sare lakini nimepnda jinsi tulivyocheza. Kwa muda mfupi wachezaji wameweza kuyashika mafunzo tuliyowapa hilo ni jambo chanya kwangu," amesema Cadena.
Akizungumzia mabadiliko ya kuingiza washambuliaji wote kipindi cha pili Cadena amesema "ilikuwa lazima nifanye vile sababu Namungo walikuwa nyuma muda mrefu na walikuwa wanaacha nafasi hivyo nilitaka tuzitumie."