Simba Sports Club
News

Cadena: Bado tuna nafasi ya kurekebisha timu

26 Nov 2023

Cadena amesema benchi la ufundi na wachezaji wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha timu inapata ushindi lakini wakati mwingine kwenye mpira kunakuwa na matokeo yasiyotarajiwa.

Akizungumzia mchezo wa jana dhidi ya ASEC Mimosas, Cadena amesema tulicheza vizuri hasa kipindi cha kwanza na tulitengeneza nafasi lakini kosa moja tulilofanya limesababisha kuruhusu bao na huo ndio mpira.

Advertisement

"Wakati mwingine mpira una matokeo usiyoyatarajia, tumecheza vizuri lakini tumefanya kosa moja wenzetu wamelitumia wakapata bao la kusawazisha.

"Bado tuna to nafasi ya kubadili hali hii na kurudi kwenye ubora wetu na kipindi hiki tunapaswa kuwa wamoja," amesema Cadena.

Back to homepage
Share this story